Polisi nchini Kenya
inamshikilia mwanaume mmoja raia wa Uingereza kwa kuhusika na kifo
cha mpenzi wake mwenye maradhi ya kisukari, baada ya kuziflashi
chooni dawa zake katika nyumba wanaoishi iliyopo Gachie, Jijini
Nairobi.
Kwa mujibu wa polisi
Muingereza huyo Carl Cary Singleton mwenye umri wa miaka 41,
aliteketeza dawa za mchumba wake huyo raia wa Kenya, na kumzuia ndani
ya nyumba hiyo kwa siku mbili baada ya kumpiga.
Vyombo vya habari vya
Uingereza vimesema Singleton walijuana kwa mara ya kwanza na mpenzi
wake huyo Peris Ashley Agumbi Mumtah aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu cha
Nairobi kampasi ya Lower Kabete kwa njia ya mawasiliano ya Facebook.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni