Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF)
limesema wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wamechoma moto ndege ya
kivita ya Kenya iliyoanguka nchini Somalia.
Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji
wa KDF, Kanali David Obonyo imesema hatma ya rubani wa ndege hiyo
haijulikani.
Taarifa hiyo imesema ni jambo la
kujutia kwa ndege hiyo kuanguka katika eneo la maadui, na al-Shabaab
kuwahi katika tukio na kuichoma moto.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni