.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Desemba 2014

COASTAL UNION KUKIPIGA NA MOMBASA COMBAIN KESHO NCHINI KENYA

TIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya”wanatarajia kusafiriki kuelekea
nchini Kenya kesho kucheza mechi ya Kirafiki na Mombasa Combaini ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania
bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa soka Manispaa ya
Mombasa ambao unaatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na joto
lililopo mjini Mombasa kuelekea mechi hiyo.

Akizungumza leo, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosu
biriwa ni siku ya mechi hiyo ambayo ni kesho.

Assenga amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ni kipimo tosha kwa Kocha Mpya
wa timu hiyo,James Nandwa kuangalia kiwango cha timu hiyo kabla ya
kuwavaa wapinzani wao Tanzania Prison.

Hata hiyo amesema kuwa licha ya kocha huyo kuangalia kiwango cha
wachezaji ambapo mechi hiyo itakuwa ni ya pili kusimama kwenye bechi
ya kwanza ilikuwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui ya
shinyanga.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni