.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Desemba 2014

MH MWIGULU NCHEMBA NA DR KAMAN WAIPA USHINDI WA KISHINDO CCM WILAYANI BUSEGA


Naibu Waziri wa Fedha ambaye pia ni Naibi Katibu Mkuu wa CCM Mh Mwigulu Nchemba kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kamani wamefanikiwa kukipa chama cha mapinduzi CCM ushindi mnono katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Nchemba na Kamani walifanya kampeni zao kwa kukinadi chama chao katika kijiji cha Nyamikoma kata ya Kabita wilayani Busega ambapo waheshimiwa hao wote kwa pamoja walivamia wilaya hiyo wakiwa na helikopta.

Wilaya ya Busega ina jumla ya vijiji 59, na katika ujumla wa vijiji hivyo CCM imeweza kupata ushindi wa vijiji 39 sawa na asilimia 66, huku Chadema wakiwa na vijiji 12, Cuf 3, Udp 4 na Act 1 vyote sawa na asilimia 34. Upande wa vitongoji viko 363, CCM vitongoji 267 sawa na asilimia 78, Chadema 73, Cuf 12, Udp 8 na Act 2 sawa na asilimia 22.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kuisha kwa uchaguzi huo, Nchemba anasema kuwa huu ni mwanzo tu, na sasa wananchi wanatakiwa kuweza kuipa nafasi ya kuweza kuongoza tena nchi hii kwani ccm ndiyo chama pekee kilichojaa amani, upendo na ushirikiano katika nchi hii.

Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa, nchi nyingi zinakuja Tanzania kujifunza namna CCM inavyoweza kuwaongoza wananchi wa Tanzania na hata kufanikiwa katika kufanikisha malengo na matakwa ya wananchi kwa wakati.

Kwa upande wake Waziri Kaman anasema kuwa, ujio wa Nchemba katika wilaya hiyo imeweza kufanikisha ushindi wa ccm ndani ya wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla .

Pia Dr Kaman alitoa pongezi za dhati kwa wananchi wa busega kwa kuweza kuipa ushindi ccm na kuweza kuwapa ahadi kubwa zaidi za kimaendeleo jimbo kwake busega.
                                                                                  Dr Kaman akiwahutubia wananchi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni