Serikali ya jimbo India imesitisha
zoezi la kufunga kizazi katika kambi maalum baada ya daktari kukutwa
akitumia pampu ya kujazia upepo matairi ya baiskeli, kujaza upepo
kwenye tumbo la mwanamke.
Daktari huyo Mahesh Chandra Rout,
ambaye alitumia pampu hiyo kujaza upepo matumbo ya wanawake 56,
Ijumaa iliyopita alinukuliwa akisema kifaa hicho kimekuwa kikitumika
mara kwa mara katika eneo la Orissa.
Maafisa wa serikali wamesema hewa ya
carbon dioxide ndio inapaswa kutumiwa kwa zoezi la ufungaji kizazi
wanawake na kuongeza kuwa kutumia pampu ya baiskeli inaweza
kuhatarisha maisha.
Mwezi uliopita kashfa nyingine
iliibuka baada ya wanawake 15 kufariki dunia baada ya kufanyiwa
kizembe upasuaji wa kufunga uzazi katika jimbo jingine.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni