Daktari wa Uganda aliyepata
maambukizi ya Ebola nchini Sierra Leone amepona na kutoka katika
hospitali aliyokuwa amelazwa nchini Ujerumani, baada ya wiki saba za
matibabu katika hospitali hiyo huko Frankfurt.
Daktari huyo aliyeajiriwa na taasisi
ya misaada ya Italia, alikuwa amelazwa Oktoba 3, katika kitengo cha
pekee cha magonjwa ya kuambukizwa cha Hospitali ya Chuo kikuu cha
Frankfurt, na aliruhusiwa Novemba 19.
Daktari huyo alikuwa amepata tatizo
la viungo vyake kadhaa vya mwili kushindwa kufanyakazi, na alikuwa
anahitaji kubadilishiwa viungo vya mwili, na sasa amepona na kuungana
na familia yake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni