Kamandi ya Jeshi la Marekani katika
bara la Afrika imesema wapiganaji wa kundi la Dola ya Kiislam (IS)
wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya.
Jenerali David Rodriguez amesema
kuna mamia ya wapiganaji wa IS ambao wanapatiwa mafunzo kwenye kambi
hizo.
Amesema kuwa kambi hizo ndio kwanza
zimeanza kutoa mafunzo, na Marekani inazifuatilia kuona namna
zitakavyoendelea.
Nchi ya Libya imetumbukia katika
machafuko tangu kiongozi wa taifa hilo Muammar Gaddafi ang'olewe
madarakani na kuuwawa mwaka 2011, huku makabila kadhaa, wapiganaji na
wanasiasa wakigombea madaraka.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni