Maandamano yameendelea kufanyika kwa
siku ya pili kufuatia kifo cha mwanaume mweusi kilichotokana na
kukabwa kooni na polisi mweupe Jijini New York.
Maelfu ya watu wameingia barabarani
Jijini New York, pamoja na katika miji mingine ya Marekani na
kusababisha foleni na watu kukaa barabarani.
Maandamano hayo yaliyoanza Jumatano,
baada ya mahakama kuamua kutomfungulia mashtaka askari aliyemuua Eric
Garner, kwa kumkaba koo.
Wanaharakati wamewekeza matumaini
yao katika uamuzi wa serikali ya jimbo kutaka kufanyika uchunguzi wa
tukio hilo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni