.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 5 Desemba 2014

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZNZ ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA HOTELI YA PARK HYATT ILIYOPO FORODHANI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar Nd. Said Sarboko Makarani akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hatua zilizochukuliwa za kuheshimu hifadhi ya urithi wa Kimataifa wakati wa ujenzi wa Hoteli ya Park Hyatt iliyopo Forodhani Mjini Zanzibar. Nyuma ya Nd. Sarboko ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Ardhi, Maji Nishati na Madini Mh. Haji Mwadini pamoja na Mratibu wa Mradi wa Hoteli ya Park Hyatt Bwana Yaqoub Osman.
Balozi Seif akikagua moja ya vyumba vya watu Mashuhuri { VIP } kwenye Hoteli ya Park Hyatt na kuridhika na kiwango kilichofikiwa. Hoteli hiyo inatarajiwa kufunguli wa rasmi kwenye shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar zinazotarajiwa kuanza rasmi mapema mwezi ujao wa Januari 2015.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkonhwe Zanzibar Nd. Said Sarboko Makarani akikagua hitimisho la ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Park Hyatt hapo Forodhani Mjini Zanzibar.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni