Aliyekuwa Naibu Rais wa Afrika
Kusini, Phumzile Mlambo-Ngcuka anaamini kuwa uongozi wa Nelson
Mandela kama kiunganisha wa kisiasa unahitajika hivi sasa Afrika
Kusini kuliko wakati wowote ule.
Mlambo-Ngcuka ambaye hivi sasa ni
Mkurugenzi wa Wanawake katika Umoja wa Mataifa amewataka wanasiasa
kufuata misingi ya Madiba katika kushughulikia mambo yanayowagawa
wananchi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea uhusiano wa umoja huyo na Mandela na
kumbukumbu alizoacha wakati dunia ikiadhimisha mwaka mmoja tangu
kiongozi huyo afariki dunia.
Uhusiano na Mandela uliimarishwa
zaidi na Umoja wa Mataifa, pale wakati Baraza Kuu la umoja huo
lilipotangaza Julai 18, kuwa siku ya Kimataifa ya kumuenzi Mzee
Nelson Mandela.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni