Nchi ya Marekani imesema imefanya
mashambulizi ya anga kwa wapiganaji wa kundi la al-Shabaab nchini
Somalia.
Mashambulizi hayo yamemlenga
kiongozi mwandamizi wa kundi hilo, katika eneo la Saakow, kwa mujibu
wa taarifa ya Idara ya Ulinzi ya Marekani.
Marekani imekuwa ikiunga mkono
jitihada za vikosi vya Umoja wa Afrika ambavyo vimewaondoa al-Shabaab
katika mji mkuu wa Mogadishu na katika miji mingine tangu mwaka 2011.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni