.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 31 Desemba 2014

MIILI YA KWANZA YA WALIOKUFA KWA AJALI YA NDEGE YAWASILI SURABAYA

Miili miwili ya kwanza kutoka ndege ya AirAsia namba QZ8501 iliyoanguka imewasili katika mji wa Surabaya nchini Indonesia ambako ndugu wanangojea.

Ndugu wa karibu wameomba kufanyiwa vipimo vya DNA, ili kusaidia kubaini miili ya ndugu zao waliokufa.

Ndege hiyo aina ya A320-200, ikiwa na abiria 162 wakitokea Surabaya kwenda Singapore, ilitoweka siku ya jumapili, na mabaki yake kuonekana baharini siku ya jumanne.

Mamlaka ya Indonesia imesema miili saba zaidi imeopolewa, lakini zoezi hilo limeathiriwa mno na hali mbaya ya hewa.
           Miili hiyo ikiwa imebebwa kwenye majeneza yaliyopewa namba 001 na 002
Awali miili hiyo ilisafirishwa kwenye mifuko ya plastiki kutoka baharini hadi katika uwanja wa ndege wa karibu wa jeshi, na kisha kuwekwa kwenye majeneza ya mbao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni