Mwanamke mmoja katika jimbo la Idaho
nchini Marekani ameuwawa na mtoto wake wa kiume wa miaka miwili kwa
kumpiga risasi baada ya kuchukua bastola kwenye pochi yake.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa
jina la Veronica J Rutledge, mwenye umri wa miaka 29, alipigwa risasi
na mtoto wake huyo kwenye duka la Wal-Mart katika mji Hayden.
Msemaji wa duka hilo amesema
mwanamke huyo alikuwa anafanya manunuzi akiwa na watoto kadhaa wakati
wa tukio hilo. Maafisa wamesema marehemu kibali chake cha silaha
kilikuwa kimefutwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni