Mwanaharakati wa Bahraini, Zainab
al-Khawaja amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuchana
picha ya Mfalme Hamad wa nchi hiyo.
Mahakama imempa fursa mwanaharakati
huyo kulipa faini ili awe huru wakati akingojea rufaa yake dhidi ya
hukumu hiyo.
Bi. Khawaja, ambaye anatokea kwenye
familia ambayo inapinga mamlaka ya nchi, anakabiliwa na kesi nyingine
wiki ijayo.
Shirika la Amnesty International
limesema litamchukulia Bi. Khawaja kama mfungwa aliyetiwa hatiani
kimakosa, iwapo ataswekwa jela.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni