.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 31 Desemba 2014

RAIS WA GAMBIA ASEMA BADO ANASHIKILIA MADARAKA YA NCHI HIYO BAADA YA JARIBIO LA KUMPINDUA

Rais wa Gambia amesema bado anashikilia mamlaka na taifa hilo la Afrika Magharibi, baada maafisa usalama wake kuzima jaribio la kumpindua.

Rais Yahya Jammeh amesema kamanda wa zamani wa jeshi alitaka kutwaa madaraka ya nchi hiyo kwa nguvu wakati akiwa ziarani nchini Ufaransa, hata hivyo hatma ya kamanda huyo haijulikani.

Awali kulikuwapo na milio mizito ya risasa karibu na Ikulu ya rais huyo katika mji mkuu.

Rais Jammeh alitwaa madaraka ya Gambia kwa mapinduzi mwaka 1994, na wakosoaji wake wanamlaumu kwa kuiongoza nchi hiyo kwa utawala wa mkono wa chuma.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni