Serikali ya Ufaransa imesema idadi
ya magari yanayochomwa moto nchini humo katika usiku wa mwaka mpya
imepungua mno.
Uchomaji moto magari umepungua kwa
asilimia 12, ikilinganishwa na mwaka 2013, matukio ambayo yamekuwa ni
desturi kufanyika kila mwaka usiku wa mwaka mpya tangu, kutokea kwa
ghasia za mwaka 2005 katika kitongoji kimoja Jijini Paris.
Idadi ya magari yaliyochomwa moto
usiku wa mwaka mpya imeshuka kutoka magari 1,067 mwaka uliopita hadi
kufikia magari 940 usiku wa kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, hali
iliyochangiwa na ulinzi mkali uliokuwepo kudhibiti uchomaji moto
magari.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni