Wanaharakati wamesema kuwa mwaka
2014 ulikuwa ni mwaka mbaya kwa nchi ya Syria katika miaka minne ya
machafuko nchini humo ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya
76,000.
Shirika la Uangalizi wa Haki za
Binadamu lenye Makao yake Uingereza, limesema raia 17,790 wameuwawa
nchini Syria wakiwemo watoto 3,501.
Wakati huo huo zaidi ya watu 15,000
wamekufa katika mapigano nchini Irak mwaka 2014 na kufanya mwaka jana
kuwa mwaka mbaya kuwahi kutokea tangu mwaka 2007.
Vingi vya vifo na machafuko hayo
vimechangiwa na wapiganaji wa kundi la Dola ya Kiislam pamoja na
vikundi vingine vya wanamgambo katika nchi za Syria na Irak.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni