Ndugu wa mmoja kati ya waandishi
wawili wa kituo cha al-Jazeera waliohukumiwa kifungo nchini Misri,
Peter Greste wamesema watamshinikiza rais kutumia mamlaka yake ili
aamuru kuachiwa kwake.
Wamesema watatoa hoja ya kumtaka
rais wa Misri kutumia mamalaka yake aliyoyatumia mwaka jana katika
kuwasafirisha kwao wafungwa raia wa kigeni ama washtakiwa wa kigeni.
Ndugu hao wa kiume wa Greste,
wamesema wamechukizwa na hatua ya ndugu yao huyo na washtakiwa
wenzake wawili kutoachiwa huru na mahakama siku ya jana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni