Mabao kutoka kwa Kane katika dakika za 30 na 52, bao la Rose katika dakika ya 44, bao la Townsend katika dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati na bao la tano toka Chadli dakika ya 78 yalitosha kabisa kukisambaratisha kikosi cha kocha msema hovyo, Jose Mourinho.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Diego Costa katika dakika ya 18, bao la pili likawekwa kimiani na Eden Hazard katika dakika ya 61 na bao la tatu likafungwa na John Terry katika dakika ya 87.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, mabingwa watetezi Manchester City wameendeleza harakati zao za kuhakikisha hawalipotezi kombe hilo baada ya kuifunga Sunderland kwa jumla ya mabao 3-2.
Mabao ya Man City yaliwekwa kimiani na Yaya Toure dakika ya 56, bao la pili likafungwa na Jovetic dakika ya 66 na bao la ushindi likawekwa kimiani na Frank Lampard dakika ya 73.
Mabao ya Sunderland yalifungwa na Rodwell dakika ya 68 na bao la pili likafungwa na Johnson kwa penati katika dakika ya 72.
Wao Liverpool jana katika ligi kuu Uingereza walijikuta na wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Leicester.
Mabao yote mawili ya Liverpool yalifungwa na Steven Gerrard kwa njia ya penati katika dakika za 17 na 40.
Sunderland mabao yake ya kusawazisha yaliwekwa kimiani na Nugent dakika ya 58 na Schlupp dakika ya 60.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, washika bunduki wa London, Arsenal walijikuta silaha zao zikishindwa kutoa risasi baada ya kushuhudia ikipata kipigo toka kwa Southampton cha mabao 2-0.
Mabao ya wenyeji hao yalipatikana kupitia kwa wachezaji Sadio Mane na Dusan Tadic.
Kwa matokeo ya michezo ya jana, Chelsea wapo kileleni wakiwa na pointi 46 sawa na Manchester City walio nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu wapo Manchester United wakiwa na pointi 37 na nafasi ya nne wamesimama Southampton wakiwa na pointi 36.
Nafasi ya tano wapo Tottenham wenye pointi 34 wakati Arsenal wapo nafasi ya sita wakiwa na pointi 33.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni