.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 6 Januari 2015

MEYA WA NEW YORK AWAKOSOA POLISI WALIOMSUSIA KUMSIKILIZA

Meya wa Jiji la New York amewakosoa vikali mamia ya polisi wa jiji hilo ambao waligeuka na kumpa mgongo wakati akiongea katika maziko ya maafisa polisi wawili.

Meya Bill de Blasio amesema kitendo cha kumsusia kiongozi mbele ya umma ni sawa na kutoonyesha heshima kwa familia za askari hao waliokufa na kwa jiji hilo.

Maafisa polisi Wenjian Liu na Rafael Ramos walipigwa risasi na kufa mwezi uliopita na mtu mwenye silaha aliyekuwa akilipa kisasi kwa polisi.

Maafisa wengi wa polisi wamekuwa wakipinga kitendo cha meya huyo, kuonyesha huruma kwa waandamanaji wanaopinga vitendo vya polisi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni