Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Wanaume wawili wamefunguliwa
mashtaka nchini Marekani kwa kujaribu kumg'oa madarakani rais wa
Gambia, Yahya Jammeh, idara ya sheria ya nchi hiyo imesema.
Washtakiwa hao ambao wanaasili ya
Gambia, wanatuhumiwa kwa kula njama za kuleta madhara kwa taifa
rafiki, pamoja na njama za kumiliki silaha.
Mamlaka za Gambia zimesema
zimefanikiwa kuzima jaribio la kuipindua serikali lililofanywa
Desemba 30, mwaka jana.
Rais Jammeh alichukua madaraka
katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi, mwaka 1994, na amekuwa
akilalamikiwa kwa kujipatia mamlaka makubwa mno.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni