Jaycee Chan, mtoto wa nyota wa
filamu Jackie Chan, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa
makosa la dawa za kulevya.
Chan mwenye umri wa miaka 32,
alikiri kosa la kutoka eneo la kutumia dawa hizo katika mahakama ya
wilaya ya Dongcheng, huko Beijing.
Polisi walivamia nyumba yake Agosti
mwaka jana na kukuta zaidi ya gramu 100 za bangi. Jaycee Chan alikuwa
anakabiliwa na kifungo kisichozidi miaka mitatu jela.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni