Mwanaume mmoja wa Florida Marekani
amefunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya polisi kueleza kuwa alimtupa
kutoka juu ya daraja mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano
katika eneo la Saint Petersburg.
Afisa wa polisi mmoja aliona tukio
hilo baada ya kumfuatilia baba huyi John Jonchuck Junior, kwa
kuendesha gari kasi, Mkuu wa Polisi Anthony Holloway ameeleza.
Mtoto huyo aliyetupwa kutoka kwenye
daraja lenye urefu wa mita 18 lenya maji alipatikana baada ya saa
mmoja na kuthibitishwa kuwa amefariki dunia baada ya kufikishwa
hospitali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni