Operesheni kubwa ya polisi
inafanyika kaskazini mashariki mwa Paris katika kuwatafuta watuhumiwa
wakuu wa mauaji yaliyotokea jumatano, katika ofisi za jarida la
vibonzo la Charlie Hebdo.
Maafisa polisi wanafanya msako
katika maeneo karibu na mji wa Villers-Cotterets ambao watuhumiwa hao
wawili ndugu waliouwa watu 12, waliripotiwa kuiba katika kituo cha
mafuta.
Wanakijiji wa kijiji cha Longpont
walizuiliwa kutoka wakati wa msako wa nyumba kwa nyumba unaowatafuta
wauaji hao ndugu Cherif na Said Kouachi.
Wanaume wakiwa kazini kuwasaka wahalifu Cherif na Said Kouachi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni