Staa wa Luninga anayetamba na kipindi cha Keeping Up With The Kardashian, mwanadada Kim Kardashian ameibuka na kusema kuwa hana mgogoro na mumewe hata kidogo.
Katika kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015, Kim ( 34 ) ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa, anachukuzwa na uvumi unaoenea kwamba yeye na mumewe Kanye West ambaye ni mwanamuziki kuwa wana matatizo katika ndoa yao.
Kim amesema kuwa anataka kukanusha uvumi huo na pia amepinga tetesi zinazoenea kuwa yeye ni mjamzito kwa kusisitiza kuwa hana mimba.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni