Nchi ya Libya imeliomba Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa, kuondoa vikwazo vya silaha ili iweze
kukabiliana na wapiganaji wa kundi la Dola ya Kislaam (IS).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya
Mohammed al-Dairi amesema kuondolewa vikwazo kutasaidia serikali
kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ugaidi.
Misri imesema inaunga mkono ombi la
Libya, katika mkutano huo wa dharura wa baraza la Umoja wa Mataifa,
uliofanyika jana.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni