Watu 37 wamekufa katika mashambulizi
ya anga yaliyofanywa kusini mwa Niger kwa kundi la watu waliokuwa
mazishi.
Tukio hilo limetokea katika kijiji
cha Abadam kinachopakana na Nigeria, ambapo ndege ambayo
haijafahamika ni ya nchi gani ilipowadondoshea mabomu.
Hali hiyo imetokea wakati Nigeria
ikisema zaidi ya wapiganaji 300 wameuwawa karibu na kusini-mashariki
mwa Nigeria katika operesheni ya kutokomeza kundi la Boko Haram.
Wakati huo huo wanajeshi wawili
wamepoteza maisha yao na wengine 10 wamejeruhiwa katika jimbo la
Borno.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni