Spika wa Bunge la Afrika Kusini
ameomba radhi kwa kumuita mende mbunge wa kambi ya upinzani.
Spika Baleka Mbete ameomba radhi
katika mkutano wa chama cha ANC, baada ya kumuamuru Kiongozi wa chama
cha EFF Malema na wabunge wa chama chake kutoka nje bungeni.
Bw. Malema alitolewa bungeni wakati
akipinga hotuba ya rais Jacob Zuma kwa taifa aliyokuwa akiitoa
bungeni.
Bw. Malema amedai kuwa kauli ya
Spika Mbete ni tishio, kwani inajulikana watu wanajua walichofanywa
watu walioitwa mende nchini Rwanda.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni