Rais Barack Obama amesema Marekani
haipigani vita na Uislam, ila ipo katika vita dhidi na watu
wanaofanya vitendo visivyokubalika na Uislam.
Obama ametoa kauli hiyo mbele ya
wawakilishi 60 wa mataifa mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa siku
tatu wa kukabiliana na makundi yenye kufuata itikadi kali, kufuatia
mashambulio ya nchini Denmark na Ufaransa.
Amesema kuwa dunia inapaswa
kupambana na itikadi zinazowafanya watu kuwa na misimamo mikali yenye
kuleta madhara.
Rais Obama amesema vikundi kama Dola
ya Kiislam na kundi la al-Qaeda si vya kidini bali ni vya kigaidi.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni