Wazazi wa wanafunzi 43 raia wa
Mexico ambao hawajulikani walipo kwa kipindi cha miezi mitano
iliyopita wameongoza maandamano makubwa katika jiji la Mexico City
wakiitaka mamlaka kufanya uchunguzi kamili.
Maelfu ya watu katika mji huo
walishiriki maandamano wakiwa wamebeba mabango yenye picha za
wanafunzui hao wa chuo cha ualimu.
Waendesha mashitaka wanasema
wanafunzi hao walikamatwa na polisi wala rushwa baad ya wanafunzi hao
kuandamana katika mji wa Iguala mnamo Septemba 26 na inasemekana
walikabidhiwa kwa genge la wahalifu ambalo liliwauwa wanafunzi hao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni