.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 4 Machi 2015

BONDIA OMARI KIMWERI AMPIGA TAFU YA VIFAA KOCHA SUPER D


Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania, kushoto bondia Omari Kimweri na kocha wa kimataifa wa mchezo wea masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakiwa na glove walizo mkabidhi kocha huyo mda mfupi kabla ya kupanda ndege na kurudi kwao Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania, kushoto akimkabidhi glove kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati ni bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchiniAustralia, Omari Kimweri ambaye aliongozana nchini na mwanasoka huyo muda mfupi kabla awajapanda ndege kurudi kwao Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi nchini Australia amempiga tafu ya vifaa vya kufundishia kocha wa kimataifa wa mchechezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
wakati wa ziara yake ya wiki mbili ya kutembelea nyumbani kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu zitumiwazo na mabondia wa nje

Kabla ya hapo bondia huyo aliongea na wadau mbalimbali wa masumbwi wakati wa mchezo wa ngumi za kulipwa kati ya Iddi Bonge na Alphonce Mchumiatumbo mpambano uliofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kumvalisha mkata wa ubingwa bondia wa uzito wa juu Mchumiatumbo baada ya kuibuka na ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza siku hiyo pia alimpiga tafu kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kwa kumkabidhi vifaa vipya vya kufundishia mchezo wa masumbwi.



Akizungumza baada ya kumkabidhi vifaa kocha Super D, alisema amekumbuka nyumbani kwa kuwa ndio alipozaliwa na kitovu chake kimezikiwa hapa nchini, hivyo ataendelea kuwakumbuka zaidi kwa kuwawezesha mabondia kucheza mara kwa mara pindi atakapoanzisha Kimweri Promotioon itakayoshilikiana na Super D Boxing Coach And Promotion kwa kushilikiana kuwapatia mabondia kupigana ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea kipato pamoja na kupandishe rekodi zao kwa mabondia chipkizi
 

Nae kocha Super D alishukulu kwa kukabidhiwa vifaa hivyo ambavyo vitamsaidia kuendelea kuinua mabondia mbalimbali chipkizi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni