Raia wa China ambaye ni meneja wa
hoteli iliyogubikwa na kashfa ya ubaguzi wa rangi nchini Kenya
ameachiwa kwa dhamana.
Meneja huyo Zhao Yang ameachiwa
baada ya upande wa mashtaka kuondoa pingamizi la dhamana waliloweka.
Mahakama imemuachia Zhao Yang kwa
dhamana ua shilingi laki moja za Kenya, wakati akingojea kusikilizwa
kesi yake.
Meneja huyo pia anashtakiwa kwa
kuishi Kenya kinyume na sheria, ambapo alikaa rumande kwa siku tatu
katika gereza la wanawake la Langata.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni