Matokeo ya awali ya uchaguzi wa
urais nchini Nigeria yanaonyesha kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini
humo Muhammadu Buhari anaongoza kidogo dhidi ya rais aliyemadarakani
Goodluck Jonathan.
Baada ya nusu ya majimbo 36 nchini
humo yakiwa yameshatangaza matokeo yake, Jenerali Buhari wa chama cha
All Progressives Congress (APC) anaongoza kwa kura nusu milioni.
Iwapo Jenerali Buhari ataibuka
mshindi atamfanya rais Jonathan kuwa rais wa kwanza aliyemadarakani
kupoteza uchaguzi katika historia ya Nigeria.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo ambao
unaushindani mkali yanatarajiwa kutolewa baadae leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni