Polisi nchini Ufaransa wamebaini
miili ya watoto wachanga watano katika nyumba moja kusini mashariki
mwa nchi hiyo, tukio ambalo linaelezwa kuwa ni baya kuwahi kutokea
katika nchi hiyo katika kipindi cha miaka mitano.
Baada ya kupatikana kwa mwili wa
mtoto mchanga mmoja kwenye mfuko wa plastiki, polisi walifanikiwa
kupata miili mingine minne ya watoto walipofanya upekuzi kwenye
nyumba moja huko Louchats, karibu na mji wa Bordeaux.
Baba mwenye umri wa miaka 40
anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo pia mama wa
miaka 35 amelazwa hospitali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni