.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 19 Machi 2015

RAIS KIKWETE AWASILI BURUNDI KULIHUTUBIA BUNGE LA EAC

Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea heshima wakati nyimbo za Taifa za nchi zao zikipigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya Jumatano, Machi 18, 2015 amewasili nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mji mkuu wa Burundi wa Bujumbura, Rais Kikwete amepokelewa na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza na pamoja na mamia kwa mamia ya wananchi wa Burundi.

Rais Kikwete ambaye amewasili Burundi akitokea Dodoma ambako alikuwa katika ziara ya kikazi pia leo Machi 19, 2015, atahutubia Bunge la Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki (EALA) katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) katika hotuba ya The State of the East African Community Address.

Saa chache baada ya kuwasili Bujumbura, Rais Kikwete amehudhuria chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Rais Nkurunzinza kwenye Hoteli ya Panoramique.

Wabunge wa Bunge la EALA pia wamehudhuria chakula hicho cha jioni.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni