.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Machi 2015

RAIS YOWERI MUSEVENI AFANYA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza baraza jipya la mawaziri hapo jana huku Mary Karooro Okurut akiteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi kuchukua nafasi ya Muruli Mukasa.

Katika mabadiliko hayo mapya, Muruli Mukasa sasa ni Waziri Jinsia, Ajira na Masuala ya Jamii nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Okurut, naye Jim Muhwezi ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari kuchukua nafasi ya Rose Namayanja.

Matia Kasaija amekuwa Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi na kuchukua nafasi ya Maria Kiwanuka ambaye anakuwa ni Mshauri Mwandamizi wa rais masuala ya Fedha, pia Peter Nyombi ameondolewa katika nafasi ya Mwanasheria Mkuu na nafasi yake kupewa Fred Ruhindi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni