Vyama vitano vya upinzani nchini
Lesotho, vimeunda muungano mpya wa kuunda serikali baada ya uchaguzi
wa dharura uliofanyika mwishoni mwa wiki kushindwa kumpata mshindi.
Uchaguzi huo uliitishwa kujaribu
kuzima hali ya hofu, baada ya kuwepo jaribio la kuipindua serikali
mwezi Agosti mwaka jana.
Waziri Mkuu anayeondoka madarakani
wa Chama cha Basotho, Thomas Thobane amekuwa wa pili kwa kupata viti
46 katika uchaguzi huo, huku Pakalitha Mosisili wa chama cha
Democratic Congress akipata viti 47 na ameungana na vyama vingine
vidogo kupata viti 61.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni