.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 5 Machi 2015

WAZIRI MKUU AZINDUA TAARIFA YA BRN

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa
sekta na miradi inayotambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo wa Tekeleza
kwa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now au BRN) ni ile yenye manufaa
makubwa nay a haraka kwa wananchi walio wengi.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) wakati akizungumza wa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya mwaka wa kwanza ya utekelezaji wa Mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa kwenye uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Vigezo hivi ndivyo vilivyotumika kutambua sekta sita za mwanzo ambazo
ni kilimo, elimu, nishati, uchukuzi, utafutaji rasilmali fedha na maji ambazo leo ndiyo tunapokea taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka wa kwanza,” alisema.

Alisema vigezo hivyo pia vilitumika kuchagua mazingira ya biasharana huduma za afya kuziingiza kwenye utaratibu wa BRN. “Serikali inaamini
kwamba kuimarika kwa mazingira ya biashara, hasa biashara ndogondogo,
kutatoa fursa za watu wengi zaidi kujiajiri na kuajiri na kuajiri
wengine,” aliongeza.

Alitoa wito kwa watendaji wote kujifunza na kuutumia mfumo huo ili waweze kufikia malengo waliyojiwejkea kwa haraka zaid. “Mambo matatu yanayoupa mfumo huu uwezo mkubwa zaidi ni kupanga kipaumbele; kuwa na nidhamu na uwazi; na haya mambo yako ndani ya uwezo wa kila Mmoja wetu ,” alisema.

Alisema Serkali itaendelea kuchukulia utekelezaji wa mfumo wa Tekeleza
kwa Matokeo Makubwa Sasa kama jambo la kipaumbele katika kutekeleza
majukumu yake.

“Haitoshi kwamba tumepata mafanikio haya katika mwaka Mmoja. Ni lazima
sasa tuazimie sote kuchukua kanuni hizi na kuzitumia katika kila eneo la maisha yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tumetoa mchango kamili kwa Taifa letu kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ta Maendeleo hadi mwaka 2015,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwashukuru Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri kwa kusimamia vema
utekelezaji wa BRN katika maeneo yao.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuukuzungumza na washiriki kabla ya
kuzindua taarifa hiyo, Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau,
Prof. Issa Omari alisema utoaji wa taarifa hiyo ni hatua mojawapo kati
ya hatua nane za mfumo huo. Aliwataka watendaji wanaotekeleza mfumo
huo wahakikishe wanafuata hatua zote nane.

Alisema kwamba jambo msingi katika utekelezaji wa BRN ni kubadilisha
maisha ya wananchi na siyo tu kupima utendaji kazi wa mawaziri wa
sekta husika.

Alisema mojawapo ya mafanikio ya utekelezaji wa mfumo huo ndani ya mwaka mmoja ni ushirikishwaji wa jamii kwa kiwango kikubwa kiasi cha kusaidia kasoro za kijamii. “Kwa mfano katika sekta ya elimu, watu wanashangaa ufaulu kupanda haraka… lakini tuna shuhuda za utoro kupungua kwenye shule moja kutpoka watoto 500 hadi sifuri…. Hii ni kwa sababu tuliishirikisha jamii hadi ngazi ya chini,” alisema.

Waziri Mkuu ameenda Kahama, mkoani Shinyanga kuwapa pole waathirika wa maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana. Mvua hiyo
imesababisha vifo vya watu 92 na kujeruhi watu 98 huku mamia watu wakiwa hawana mahali pa kuishi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni