Idadi ya vifo vya watu waliokufa
katika tukio la watu wenye silaha kushambulia Chuo Kikuu cha Garissa
kaskazini mwa Kenya leo afajiri imefikia watu 15.
Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya
limesema watu wapatao 65, wakiwemo polisi wawili wamejeruhiwa na
kukimbizwa hospitali.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa
rasmi zinasema kuwa kuna idadi ya wanafunzi kadhaa wanashikiliwa
mateka na washambuliaji hao.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni