Dereva wa mbio za Langalanga
Muingereza Lewis Hamilton ameipatia ushindi timu yake ya Mercedes katika mbio za Chinese
Grand Prix.
Muingereza huyo bingwa wa mbio hizo
wa dunia, aliongoza kwa umbali akionyesha umahiri wake na kumshinda
dereva mwenzake wa timu ya Mercedes Nico Rosberg.
Madereva wa timu ya Ferrari,
Sebastian Vettel pamoja na Kimi Raikkonen walionyesha ushindani
lakini walizidiwa na uwezo wa timu ya Mercedes wa kumudu kubadilisha
matairi.
Katika mbio hizo timu ya Williams,
yenye madereva Felipe Massa pamoja na Valtteri Bottas walishika
nafasi ya tano na ya sita.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni