Mshambuliaji nguli wa Chelsea, Didier Drogba akipiga mpira uliokwenda moja kwa moja nyavuni na ukisawazishia timu yake katika dakika ya 48 muda mfupi tu baada ya kipindi cha pili kuanza.
MBONA MWAKA HUU WETU!! Wachezaji wa Chelsea wakiwasalimia mashabiki wao baada kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Leicester na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Ligi kuu ya Uingereza imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa mchezo mmoja tu, ambapo vinara wa ligi hiyo Chelsea walikuwa ugenini kucheza na Leicester.
Katika mchezo huo, Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Hata hivyo iliwabidi vinara hao wa ligi kuu Uingereza kusubiri hadi kipindi cha pili kupata mabao yao, baada ya kutangulia kufungwa na wenyeji wao katika dakika ya 45 za kwanza bao lililofungwa na Marc Albrighton.
Kuanza kwa kipindi cha pili, Chelsea walikuja juu na kujipatia mabao yao kupitia kwa Didier Drogba dakika ya 48, John Terry akifunga bao la pili katika dakika ya 79 na Ramires akiifungia Chelsea bao la tatu nala ushindi katika dakika ya 83.
Kwa matokeo hayo, Chelsea wamefikisha pointi 80, na kama wakishinda mchezo wao unaofuata mwishoni mwa wiki wiki hii ni dhahiri watatangaza ubingwa mapema.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni