Australia imemtaka balozi wake
kuondoka nchini Indonesia baada ya raia wake wawili kuuwawa baada ya kutiwa
hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.
Raia hao Andrew Chan na Myuran
Sukumaran ni miongoni mwa watu wanane kutoka mataifa kadhaa waliouwawa kwa
kupigwa risasi hii leo katika gereza la kisiwa cha Nusakambangan.
Serikali ya Brazil nayo
imeonyesha kusikitishwa mno kutokana na kuuwawa kwa raia wake aitwae Rodrigo
Gularte.
Hata hivyo mwanamke mmoja
alisitishiwa adhabu ya kuuwawa baada ya kuelezwa kwamba mwanamkeambaye aliyemuwekea
dawa za kulevya alikuwa anashikiliwa gerezani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni