Maafisa usalama wa Marekani
wapatao 200 wamewasili nchini Kenya pamoja na magari mawili ya silaha kwa ajili
ya maandalizi ya ulinzi wa Rais Barack Obama atakayoifanya mwezi Julai.
Timu hiyo ya maafisa usalama pia
itahusika kusimamia ulinzi wa maafisa wawili waandamizi wa serikali ya Marekani
wanaotarajiwa kuwasili Kenya katika wiki ijayo.
Magari hayo yamewekwa katika
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya uliopo Gigiri, huku idadi kubwa ya maafisa
usalama wakiwa Jijini Nairobi na wengine wamepelekwa Kisumu, alikozaliwa baba
wa rais Obama.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni