Bondia Floyd Mayweather amembeza Manny
Pacquiao wakati wa kuelekea kwa pambano lao linalongojewa kwa hamu siku ya
jumamosi, kwa kumuambia anapaswa kuingiza fedha nyingi zaidi kama ilivyo yeye.
Pambano hilo ni miongoni mwa
mapambano ghali mno katika historia ya masumbwi, ambapo mabondia hao watagawana
kiasi cha dola milioni 150, ingawa kiasi halisi cha fedha hiyo hakikuwekwa
wazi.
Hata hivyo mgao wa fedha hizo
unaonyesha Mayweather atachukua asilimia 60, huku Pacquiao akiambulia asilimia
40 za fedha iliyotengwa kwa ajili ya malipo ya mabondia hao kudundana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni