Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Duniani Papa Francis ameshutumu mgawanyiko na kuwepo kwa
ukimya dhidi ya matukio ya mashambulizi ya Jihadi dhidi ya Wakristo
duniani, kauli ambayo ameitoa wakati akiongoza sherehe za Pasaka.
Kiongozi huyo wa kanisa
hilo lenye waumini wapatao bilioni 1.2 amegusia suala la mauaji ya
wakristo yanayofanywa na watu wenye itikadi kali za kidini, wakati
kanisa likisherehekea siku kuu takatifu ya Pasaka ambayo ni ya
kufufuka kwa Yesu kristo.
Katika wiki hii
takatifu kwa mujibu wa kalenda ya Kanisa, wanafunzi wakristo 152
waliuwawa katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya katika shambulio
lililofanywa na kundi la kigaidi la Somalia la al-Shabaab.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni