Afisa polisi mzungu wa South
Caroline nchini Marekani amefunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya
video kumuonyesha akimpiga risasi mgongoni na kumuua mtu mweusi
aliyekuwa akikimbia.
Afisa upelelezi wa jimbo hilo jana
amemkamata polisi huyo wa kituo cha North Charleston, aitwae Michael
Slager, baada ya kuangalia video iliyorekodiwa kwa simu ya mkononi.
Mamlaka zimesema Walter Lamer Scott
alipigwa risasi baada ya afisa polisi kumlenga na silaha ya
kusababisha shoti. Idara ya Sheria ya Marekani inatarajia kuanza
uchunguzi wa tukio hilo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni