Shirika la Kimataifa la Msalaba
Mwekundu (ICRC) linatarajia kupeleka ndege mbili za kutoa msaada wa
dharura katika mji mkuu ya Sanaa nchini Yemen.
Shirika hilo limepewa ruhusa ya
kutua ndege zake zikiwa na watumishi pamoja na dawa za matibabu
nchini Yemen ambapo inaelezwa kunahitajika misaada ya dharura ya
kibinadamu.
Mashambulizi ya anga yanayoonozwa na
nchi ya Saudi Arabia yakiwalenga waasi wa Houth, yameendelea kufanywa
kwa usiku wa 12 mfululizo.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi
ya watu 500, wameuwawa katika wiki mbili zilizopita nchini Yemen.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni