Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF Jamal Malinzi, ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa
klabu ya Simba SC Bw. Evans Aveva kufuatia vifo vya mashabiki wa
klabu hiyo, viliyotokea jana katika ajali ya barabarani eneo la
Makunganya mkoani Morogoro.
Katika salamu zake Rais Malinzi
amesema, TFF imezipokea kwa masikitiko taarifa hizo za ajali na kwa
niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, wanawapa pole wafiwa wote
na mwenyezi Mungu awape nguvu majeruhi waweze kupata nafuu na kupona
kwa uharaka zaidi.
Aidha Rais Malinzi ameagiza michezo
yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itakayochezwa wikiendi hii
nchini, kusimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka mashabiki
waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
MALINZI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS
WA FIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
TFF jana ijumaa ilipokea ugeni wa makamu wa Rais wa FIFA ambaye pia
ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Jordan, HRH Prince
Ali Bin Al Hussein. (picha ya Rais Jamal Malinzi na HRH Ali
imeambatanishwa)
Jioni Prince Ali Bin AliHussein na
ujumbe wake walifanya mazungumzo na Rais wa Shrikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF Jamal Malinzi katika hoteli ya Kilimanjaro
Kempsinki (Hyatt) iliyopo jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo, zaidi
waligusia maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya TFF na Chama cha
Mpirwa wa Miguu nchini Jordan (JFA), hasa katika maeneo ya maendeleo
ya mpira wa vijana, makocha na waamuzi.
HRH Prince Ali Bin Al Hussein ambaye
ni mgombea wa nafasi ya urais FIFA mwaka huu, ameondoka leo mchana
kurudi nyumbani kwake Jordan.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni