Mamia ya wahamiaji wa jamii ya
Rohingya na raia wa Bangladeshi wameokolewa na wavuvi katika bahari
ya Indonesia, baada ya kukaa majini tangu wiki iliyopita, huku nchi
za Malaysia na Indonesia zikikubali kutoa hifadhi ya muda.
Taarifa zinaeleza wahamiaji hao 370,
wakiwemo wanawake 50 na watoto 50 wamekuwepo baharini kwa wiki kadhaa
wakikabiliwa na njaa huku miili yao ikiwa imeishiwa na maji ambapo
pia boti yao ilikuwa ni chafu na yenye wadudu.
Wahamiaji hao wameokolewa wakati
mawaziri wa Thailand, Malaysia na Indonesia wakiitisha mkutano wa
dharura Jijiji Kuala Lumpur kujadili mgogoro unaokuwa wa janga hilo
la wahamiaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni