Jumapili, 24 Mei 2015
MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOA WA KUSINI PEMBA KUANZA MBIO ZAKE
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Juma Kassim Tindwa akisoma taarifa fupi ya mkoa wake, kabla ya kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mhe: Mwanajuma Majid Abdalla kwa ajili ya kuanza mbio zake mkoani humo, makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa ndege Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Mwanajuma Majid Abdalla akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Juma Kassim Tindwa ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba
Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiaza mbio hizo baada ya kuwasili Kisiwani Pemba katika uwanja wa ndege wa ChakeChake ukitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kukamilisha mbio zake na kuzindua miradi ya Maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huo. Mwenge huo utaaza mbio zake katika Mkoa wa Kusini Pemba na kuzinduliwa kwa miradi ya Maendeleo katika Mkoa huo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni